Kaunty ya kakamega yaanzisha mradi wa maji wa shilingi Millioni Mia Moja!

Kaunti ya kakamega imewekeza takriban shilingi milioni miamoja kwa mradi wa maji kule chekalini kaunti ndogo ya lugari ili kufanikisha usambazaji wa maji kwa wakaazi.

Gavana wa kakamega wycliff oparanya amesema mradi huo ambao tayari umeanza kukarabatiwa unalenga kuwafikia jumla ya watu 22,000 wa chekalini na baadhi ya wadi za lugari.

Akizungumza baada ya kuzuru mradi huo kudadisi ujenzi wake, oparanya amesema mradi huo utakuwa tayari kwa uzinduzi ifikapo mwezi disemba mwaka huu.

Gavana huyo amesema fedha hizo zilitumika kuchimba bwawa, kununua transfoma na halkadhalika kununua mtambo wa kusafisha maji kutoka australia aliohutaja kama wa kipekee nchini na kusema utasaidia kusambaza bidha hiyo muhimu kwa wakaazi.

Mradi wa kuhakikisha kuwa wakaazi katika kaunti hiyo wanafaidi maji safi ni baadhi ya ruwaza ya oparanya huku akisema anapania kuhakikisha mradi huo unasambazwa kwa kila eneobunge hii ikiwa njia mojawepo ya kubuni ajira na kusambazia wakaazi umeme. More

Facebook Comments Box