Video: Baba ya Caroline Kangogo anyimwa Mwili wa mwanae!

Hali ya taharuki ilishuhudiwa katika hospitali ya iten, county ya Elgeyo marakwet, baada ya mzee Barnabas Kibor, ambaye ni baba ya aliyekua Ofisa wa polisi mwenda zake Caroline Kangogo kupiga mayowe, alipofahamishwa kwamba hatapewa mwili wa mwanae.

Familia ya Caroline ilikua imefika katika hospitali hii, na walikua wanataka wapatiwe mwili, ili waweze kumpumuzisha kama ilivyopangwa.

Ilikua ni kizazaa baada ya familia hii kuarifiwa kua, hawatapewa mwili wa Kangogo kwasababu bado upasuaji haujafanywa.

Kulingana na mzee kibor, familia ilikua tayari imeshaa jipanga na maandalizi ya maziko ya mwanao, na walikua wametumia pesa nyingi kwa mpango mzima.

Caroline Kangogo almarufu kama killer cop, alpatika tarehe kumia na sita mwezi wa saba mwaka 2021, akiwa ameaga dunia, baada ya kujipiga risasi kichwani.

Bado haijulikani ni lini Familia ya Kangogo itakabithiwa mwili wa mwanao kwa maziko kwasababu bado upasuaji hujafanyika, na haijulikani ni lini utafanyika. More

Facebook Comments Box